Chelsea inautaka kweli ubingwa wa FA

Muktasari:

Chelsea inatarajiwa kumenyana na Manchester United ya Jose Mourinho katika mchezo wa fainali baada ya kuilaza Southampton ‘Watakatifu’.

LONDON, ENGLAND. NAHODHA  wa Chelsea Gary Cahill, amesema wanautaka ubingwa wa Kombe la FA ili kupunguza presha msimu huu.

Chelsea inatarajiwa kumenyana na Manchester United ya Jose Mourinho katika mchezo wa fainali baada ya kuilaza Southampton ‘Watakatifu’.

Libero huyo amesema Chelsea inatakiwa kutwaa ubingwa baada ya kupokwa Kombe la Ligi Kuu England na Manchester City.

Amesema baada ya kupoteza ubingwa wa England, jukumu lao ni kuifunga Man United katika mchezo wa fainali.

Tangu kuanza msimu huu Chelsea imeshindwa kutamba chini ya kocha Mtaliano Antonio Conte licha ya kuipa ubingwa msimu uliopita.

Cahill amesisitiza endapo Chelsea itakuwa mabingwa, itarejesha morali ya kufanya vyema katika Ligi Kuu.

“Ligi Kuu haitabiriki. Malengo yalikuwa kushinda na kutwaa ubingwa, lakini msimu huu hali imekuwa ngumu kwetu,”anasema Cahill.

Mchezaji huyo ameongeza Kombe la FA lina heshima kubwa na mashabiki wana matarajio Chelsea itawapoza machungu kwa kutwaa ubingwa.