Chelsea yakomaa kwa Batshuayi

Muktasari:

Lakini Chelsea imesisitiza, kamwe haitamwacha straika wao Michy Batshuayi kwa pesa ya mboga na watakuwa tayari kukaribisha mazungumzo kama itawekwa mezani Pauni 50 milioni.

Munich, Ujerumani. WALIMUONA wa nini pale Stamford Bridge, lakini Borussia Dortmund wakasema mleteni huku tuwaonyeshe na sasa wameelewa.

Lakini Chelsea imesisitiza, kamwe haitamwacha straika wao Michy Batshuayi kwa pesa ya mboga na watakuwa tayari kukaribisha mazungumzo kama itawekwa mezani Pauni 50 milioni.

Batshuayi yuko kwa mkopo pale Dortmund, lakini baada ya kukoshwa na kiwango chake sasa wanamtaka jumla, lakini Chelsea inataka dau hilo kwanza ndipo iweze kumuachia.

Straika huyo wa Ubelgiji, amekuwa kwenye kiwango bora zaidi baada ya kutua Bortmund, ambapo awali alionekana kuwa mzigo kwenye kikosi cha Mtaliano Antonio Conte.