Mourinho ampa ukocha Carrick

Muktasari:

Kiungo huyo kwa sasa anasubuliwa na matatizo ya moyo

London, England. Nahodha wa Manchester United, Michael Carrick atakuwa kocha wa klabu hiyo baada ya kustaafu soka mwisho wa msimu huu.
Kocha Jose Mourinho amethibisha kuwa kiungo huyo mwenye miaka 36, akatakuwa mmoja ya wasaidizi wake katika kufundisha kikosi cha kwanza cha timu hiyo baaada tu ya kustaafu.
Carrick hajacheza tangu alipopata tatizo la moyo Septemba mwaka jana.
Kiungo huyo wa England, ametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa akiwa na Man United, amekuwa akifanyiwa matatibu tangu Novemba mwaka jana.
Mourinho, alizungumzia kuhusu Carrick kuchukua jukumu la ukocha, alisema: "Klabu inafuraha kuona akiendelea kuwa hapa.
"Pia, mimi nimefuraha kusikia kwamba ataungana name hapa.
"Amekuwa nje bila ya kufanya mazoezi kwa miezi kadhaa na sasa ni wiki ya pili tangu ameanza mazoezi pamoja na timu. Ni mchezaji muhimu katika kikosi chetu.
"Nafikiri ni uamuzi mzuri kwa timu na kwake pia kuamua kustaafu soka akiwa hana majeruhi au tatizo lolote."
Carrick amefanikiwa kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu England, alipatwa na tatizo la moyo wakati wa mchezo wa Kombe la Ligi walioshinda 4-1 dhidi ya Burton uliofanyika Septemba 20 mwaka jana.