Bondia McGregor atamba kumuadhirisha Floyd Mayweather

Thursday July 13 2017

 

Marekani. Mabondia wa Marekani, Floyd  Mayweather na Conor McGregor wanatarajia kutwangana Agosti 26 katika pambano litakalopigwa jijini Los Anges.

Wababe hao walikutana juzi Jumanne kwenye Ukumbi wa Los Angel baada ya kukutanishwa na mapromota wao, hivyo walitumia fursa hiyo kuelezea mchezo wao.

McGregor aliahidi kumuadhiri mpinzani wake huku akisema Mayweather hana uzoefu kwenye mchezo huo.

Naye Mayweather alijibu kwa kusema anauhakika atamuondoa ulingoni na kurudi kwao mapema tu.