Bingwa wa Parampiki apania kuvunja rekodi iliyowekwa na Bolt

Muktasari:

Mlemavu huyo wa miguu alishinda medali za dhahabu kwenye mbio za mita 200 na 400 m katika mshindano ya Rio 2016.

London, Uingereza. Mshindi mara mbili wa mashindano ya dunia ya walemavu, Liam Malone amesema atatumia mbinu za mkongwe wa riadha Usain Bolt kwenye mashindano ya miaka mitatu inayokuja.

Mlemavu huyo wa miguu alishinda medali za dhahabu kwenye mbio za mita 200 na 400 m katika mshindano ya Rio 2016.

Mfukuza upepo raia wa Jamaica, Bolt ambaye anatarajiwa kustaafu msimu huu kwenye Mbio za Dunia wakati wa kiangazi pia ni mshindi mara nane wa Olympic.

Mwanariadha Bolt aliweka rekodi ya kukimbia mita 100 kwa sekunde 9.5 mwaka 2009.

Malone ambaye hajashiriki mashindano ya  Riadha ya Dunia kwa walemavu yanayoendelea London, ameshindwa kutokana na kuwa majeruhi na anaamini teknolojia ambayo imeboreshwa kwenye vifaa wanavyotumia wakati wa kukimbia itamwezesha kuweka rekodi mpya katika mashindano miaka mitatu ijayo.

Melone alisema lengo lake katika kipindi cha miaka mitatu ijayo lengo lake ni kufikia rekodi ya Bolt na kuipita ambapo anajifua ili kukimbia mita 100 kwa sekunde 9.4.