Bilionea Mturuki kuinunua Newcastle United

Muktasari:

Newcastle inashika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Uturuki. Bilionea Mturuki, Mfalme Murat Ulker amethibitisha kutaka kuinunua klabu ya Newcastle kutoka kwa mmiliki wake wa sasa, Mike Ashley.
Tajiri huyo wa Uturuki ameweka bayana kwamba yupo tayari kulipa Pauni 220 kwa ajili ya kuinunua hiyo ni kutokana na mmiliki huyo kutaka kuiuza klabu hiyo ya Ligi Kuu England.
Taarifa zinasema kwamba kigogo huyo amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha azma yake inatimia na ameonyesha nia jambo ambalo inaonekana huenda likakamilika hivi karibuni.
Tajiri huyo anatajwa na jarida la Forbes kuwa na akiba ya pesa kiasi cha Pauni 2.8 bilioni na anasimamia makampuni makubwa Uturuki kama vile Yildiz Holdings na mengine yanayofanya kazi barani Ulaya.