Benzema kusaini mkataba

Muktasari:

Mkataba huo utamuweka hapo kwa kipindi cha miaka minne mingine huku kukiwekwa kipengele ambacho kitamruhusu kuondoka klabuni hapo kwa dau la pauni 890 milioni kwa klabu inayomtaka.

STAA wa Real Madrid, Karim Benzema anatajirwa kusaini mkataba mpya na wababe hao wa Santiago Bernabeu.
Mkataba huo utamuweka hapo kwa kipindi cha miaka minne mingine huku kukiwekwa kipengele ambacho kitamruhusu kuondoka klabuni hapo kwa dau la pauni 890 milioni kwa klabu inayomtaka.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 29 anatazamiwa kusaini mkataba huo leo na ataendelea kukipiga klabuni hapo mpaka mwaka 2021 kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Ufaransa na Hispania.