Balotelli apigwa faini, kisa kawa kibonge

Muktasari:

Kwa mujibu wa L’Equipe, Nice hawakufurahishwa na jambo hilo kwa sababu Balotelli alikuwa ameongezeka kilo 15 kwa kipindi alichokuwa mapumziko, kwa sababu wakati anaondoka msimu ulipokwisha, alikuwa na uzito wa kilo 88.

STRAIKA Mario Balotelli amepigwa faini na klabu yake ya Nice kutokana na kuongezeka uzito.

Balotelli amedaiwa alirudi kujiunga na timu hiyo akitokea kwenye mapumziko ya mwisho wa msimu akiwa na kilo 103.

Kwa mujibu wa L’Equipe, Nice hawakufurahishwa na jambo hilo kwa sababu Balotelli alikuwa ameongezeka kilo 15 kwa kipindi alichokuwa mapumziko, kwa sababu wakati anaondoka msimu ulipokwisha, alikuwa na uzito wa kilo 88.

Amepungua kidogo msimu huu, lakini bado anapaswa kujipunguza vizuri ili kurudi kwenye makali yake kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Jambo hilo limedaiwa kuathiri kiwango chake cha msimu huu na kwenye mechi ya kimataifa ya Italia, alicheza ovyo sana dhidi ya Poland kabla ya kuwekwa benchi kwenye mechi dhidi ya Ureno.