Bakayoko hana presha kuvaa viatu vya Matic

Muktasari:

Matic, 29 aliisaidia Chelsea kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, lakini akiwa amebeba taji hilo mara mbili katika zama zake alizokuwa Stamford Bridge kabla ya kwenda kuungana na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho huko Old Trafford.

KIUNGO, Tiemoue Bakayoko amesema wala haimtii presha kuwa na kazi ya kuvaa viatu vya Nemanja Matic kwenye kikosi cha Chelsea baada ya Mserbia huyo kuhamia Manchester United kwenye dirisha lililopita.
Matic, 29 aliisaidia Chelsea kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, lakini akiwa amebeba taji hilo mara mbili katika zama zake alizokuwa Stamford Bridge kabla ya kwenda kuungana na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho huko Old Trafford.
Matic anaonekana kufanya vizuri huko kwenye klabu yake mpya ya Man United huku Bakayoko naye akipambana na hali yake hukoStamford Bridge kuhakikisha anafanya vizuri na kumpa kocha Antonio Conte kile anachotarajia kukipata kutoka kwake.