Kigogo Dortmund atua London kumalizana Arsenal

Muktasari:

Mshambuliaji huyo wa Gabon amekuwa akilazimisha kutaka kuondoka Dortmund

London, England. Mkurungezi wa Ufundi wa Borussia Dortmund, Michael Zorc amekwenda London kukamilisha uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang kwenda Arsenal.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani,  Zorc atakuwa London leo katika mazungumzo ya kuhusu uhamisho wa mshambuliaji huyo wa Dortmund anayetaka kutua Gunners.
Taarifa zinasema jadiliano hayo yatakuwa hasa kuhusu bei ambayo Arsenal wametajiwa ya pauni 53 milioni ili kumchukua  Aubameyang.
Hata hivyo, Gunners imejiweka vizuri kumnasa nyota huyo wa Gabon baada ya mshambuliaji huyo kuachwa katika kikos cha Dortmund kilichosafiri Ijumaa kucheza dhidi ya Hertha Berlin.
Arsenal wanaamini watamsajiki mshambuliaji huyo na kumuaidi mshahara wa pauni 170,000 kwa wiki. Pia uwezekano wa kumtumia Olivier Giroud kama sehemu ya uhamisho huo utaweza kuwashawishi Dortmund.