Arsenal yaonyesha makali yake msimu huu kwa Bayern Munich

Muktasari:

Arsenal katika mchezo huo wa kirafiki ilitoka sare ya 1-1 kisha kupigiana matuta na kushinda penalti 3-2  mechi iliyopigwa Shangai leo Jumatano.

Klabu ya Arsenal imeanza kulipa kisasi cha mabao 5-1 ilichopokea kutoka kwa Bayern Munich kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Arsenal katika mchezo huo wa kirafiki ilitoka sare ya 1-1 kisha kupigiana matuta na kushinda penalti 3-2  mechi iliyopigwa Shangai leo Jumatano.

Kocha Arsene Wenger alionekana kwenye benchi akishuhudia silaha zake mpya alizosajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi msimu mpya wa 2017/18.