Arsenal, City zamgombea Iniesta

Muktasari:

Kiungo wa Barcelona (33), alionyesha ubora wake wakati timu hiyo iliposhinda mabao 5-0 dhidi ya Sevilla na kunyakuwa ubingwa wa Kombe la Mfalme wiki iliyopita.

London, England. Arsenal na Manchester City ‘zinajaribu kumshawishi kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta ajiunge nayo badala ya kwenda China’.

Kiungo wa Barcelona (33), alionyesha ubora wake wakati timu hiyo iliposhinda mabao 5-0 dhidi ya Sevilla na kunyakuwa ubingwa wa Kombe la Mfalme wiki iliyopita.

Taarifa zinadai kuwa tayari kiungo huyo mkongwe amepata dili ya kupata fedha nyingi mashariki ya mbali.

Lakini gazeti la Hispania la AS limedai kuwa klabu za England, Man City na Arsenal zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo wa Nou Camp.

Hiyo ni kutokana na makocha wake wawili  wa zamani wa Barcelona kila mmoja kuonyesha nia ya kutaka huduma yake.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola aliyekuwa kocha wa Barcelona kuanzia 2008 na 2012, inadaia anamtaka Iniesta ndani ya Etihad na amekuwa akifanya jitihada kubwa kumshawishi ajiunge naye.

Pia, Luis Enrique anayepewa nafasi kubwa ya kurithi mikoa ya Arsene Wenger ndani ya Arsenal naye anataka kufanya kazi na Iniesta.