Wigan yaiduwaza Man City Kombe la FA

Muktasari:

Kutokana na vurugu hizo wachezaji wa Man City walilazimika kutolewa na uwanjani chini ya ulinzi wakati mashabiki wa Wigan walipovamia uwanja kusherekea ushindi wao wa bao 1-0 waliopata dhidi ya City.

London, England. Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero alipambana na mashabiki wa Wigan Athletic baada ya timu yake kutolewa katika mechi ya raundi ya tano ya Kombe la FA.

Kutokana na vurugu hizo wachezaji wa Man City walilazimika kutolewa na uwanjani chini ya ulinzi wakati mashabiki wa Wigan walipovamia uwanja kusherekea ushindi wao wa bao 1-0 waliopata dhidi ya City.

Picha za televisheni zilimuonyesha Aguero akirushiana makonde na mashabiki hao waliokuwa wakivamia uwanja.

Mashabiki wa kwenye Uwanja wa DW walianza kurusha mabango ya matangazo kwa polisi kabla ya kuingia uwanjani.

Mwenyekiti wa Wigan, David Sharpe aliimbia BBC Radio 5: "Si vizuri kuona mashabiki wakiwa na hisia za namna hiyo. Sikupenda kuona mechi hii ikimalizika kwa namna hii.

"Ni ushindi mkubwa, lakini tunatakiwa kuheshimu mchezo wa soka. Sijapande hiki ninachokiona hapa uwanjani."

Mchezaji wa Will Grigg alifunga bao pekee kwa Wigan inayoshiriki daraja la kwanza katika dakika 79, na kumaliza ndoto ya Man City ya kutwaa mataji manne msimu huu.

Katika mchezo huo Man City ilipata pigo baada ya mchezaji wake Fabian Delph kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Max Power katika kipindi cha kwanza.

Jambo hilo liliwafanya makocha wote wa pande zote mbili kurushiana maneno wakati wa muda wa mapumziko.