AC Milan yachekelea mauzo ya juu ya tiketi msimu huu

Muktasari:

Kampeni ya mauzo ya tiketi kwa msimu mpya wa 2017/18 ilianza kuuzwa jana Jumatatu ambapo kwa siku  hiyo ya kwanza pekee zaidi ya tiketi 30,000 ziliuzwa ikilinganisha na mwaka jana ambapo ziliuzwa tiketi 16 450 ndio ziliuzika.

Italia. Mauzo ya tiketi za klabu ya AC Milan imeripotiwa kuongezeka mara dufu ikilinganisha na siku ya kwanza ya mwaka jana.

Kampeni ya mauzo ya tiketi kwa msimu mpya wa 2017/18 ilianza kuuzwa jana Jumatatu ambapo kwa siku  hiyo ya kwanza pekee zaidi ya tiketi 30,000 ziliuzwa ikilinganisha na mwaka jana ambapo ziliuzwa tiketi 16 450 ndio ziliuzika.

Tiketi 43,140 ziliwahi kuuuzwa msimu wa 2007/08 ambapo klabu hiyo ilitwaa ubingwa wa wa Seia A.

AC Milan imemaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Seria A msimu ulioisha.