Ni vita ya Chelsea, Roma, Atletico Kundi C

Muktasari:

Mchezo huo wa Kundi C utapigwa leo Jumanne usiku na  Chelsea itahitaji ushindi au sare ili kujiweka kwenye nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.

England. Chelsea wataikaribisha Atletico Madrid kwenye mchezo wa mwisho wa makundi kufuzu hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezo huo wa Kundi C utapigwa leo Jumanne usiku na  Chelsea itahitaji ushindi au sare ili kujiweka kwenye nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.
Roma itajiweka katika mazingira na mazuri kwenye kundi hilo iwapo itashinda, huku ikiiombea Chelsea mabaya.
Atletico Madrid itahitajika kushinda iwapo inataka kusoga mbele huku nayo ikiomba dua mbaya kwa Roma ipoteze mchezo huo wa leo Jumanne.