Antonio Conte ashusha pumzi, aula mkataba wa miaka miwili Chelsea

Muktasari:

Awali, Conte alikuwa akihusishwa kurudi Italia katika msimu huu wa usajili wa kiangazi, hivyo mkataba huo mpya umemaliza tetesi hizo zilizokuwa zikiripotiwa kwenye vyombo vya habari.

London, England. Baada ya kuwa katika sintofahamu kwa muda mrefu, hatimaye Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho.

Awali, Conte alikuwa akihusishwa kurudi Italia katika msimu huu wa usajili wa kiangazi, hivyo mkataba huo mpya umemaliza tetesi hizo zilizokuwa zikiripotiwa kwenye vyombo vya habari.

Kocha huyo amesajiliwa kwa mkataba wa thamani ya Pauni 20 milioni.

Conte alisema ni jambo la furaha kwake kuongezewa mkataba na anaamini mafanikio yake aliyoyapata katika mwaka wake wa kwanza akiwa Chelsea ndiyo yamewasukuma mabosi wake kumbakiza klabuni hapo.