Tattoo ya Sterling gumzo kila kona

London, England. Nyota wa Manchester City, Raheem Sterling amesherehekea bao lake la kwanza msimu huu dhidi ya Arsenal kwa kuchora tattoo nyingine mwilini mwake.
Sterling alifunga bao hilo dakika ya 14, wakati Man City ikichapa Arsenal kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates jana Jumapili.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Sterling ameposti picha inayomuonyesha akimpiga busu mtoto wake Thiago mwenye umri wa mwaka mmoja ambayo ndiyo imetumika katika mchoro huo wa tattoo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipata mtoto huyo mwaka jana na mchumba wake wake, Paige Milian.
Sterling sasa amefikisha jumla ya mabao 50 aliyofunga katika Ligi Kuu England.