Neymar ataka aachwe ishu za usajili

Tuesday May 15 2018

 

WAKATI kocha wa Manchester United, Jose Mourinho akitenga mzigo wa Pauni200mil kuinasa saini ya Neymar mwenyewe amesema anakerwa na habari za kumuhusisha na uhamisho wakati akili yake iko Paris Saint-Germain.

Mchezaji huyo iliwahi kuripotiwa kwamba hafurahii maisha ya Ligue 1 na kwamba mpango wake ni kuondoka.

Real Madrid imekuwa ikipambana kuinasa saini ya Neymar imlete Santiago Bernabeu aunganishe nguvu na Cristiano Ronaldo.

Pia kumekuwa na ripoti kwamba Man United inataka kupimana ubavu na Madrid kuwania saini ya mchezaji huyo na kwamba wako tayarti kulipa mshahara sawa wa Pauni30 milioni kwa mwaka anaolipwa mchezaji huyo huko PSG.

Neymar alikuwa Paris juzi Jumapili akipokea Tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Ligue 1 na kusema hayo.