Waruru ajenga ukuta Kogalo

Tuesday July 4 2017

 

By Vincent Opiyo

Naambiwa Waruru lamaanisha uchungu kwa lugha ya mama kule mkoa wa kati. Ndiyo aliyoyafanya straika wa Ulinzi Stars Stephen Waruru juzi Jumapili mjini Kisumu.

Waruru alianzisha bifu ambayo kamwe haitakuja kuisha hivi karibuni. Wakati Kogalo ikidhania imeshavuna ushindi wa 2-0 ngarambe ya ligi kuu ya KPL, Waruru alifanya kitu ambacho Lionel Messi au Cristiano Ronaldo hukifanya tu.

Jamaa alirejesha magoli yote mawili chini ya dakika kumi. Ni bao la pili lilizua fujo uwanjani humo alipovua jezi na kusheherekea mbele ya halaiki ya mashabiki wa Kogalo akionyesha kidole cha kati.

Hapo ndipo alijua wafuasi walihamakishwa na kuanza kurusha mawe na vichupa uwanjani walipovutia maafisa wa usalama kulipua vitoa machozi. Mechi ikasitishwa kwa dakika kumi hivi kabla ya kumalizia dakika mbili za mwisho.

“Ni kitu ambacho sikutarajia kwa mchezaji mwenye tajiriba ya miaka mingi kama huyu. Popote ulimwenguni huwezi kufunga goli na usherehekee kwa namna ya kuudhi mbele ya mashabiki wapinzani. Alizua hasira miongoni mwao na kuchangia vurugu,” aliteta kocha wa Gor Mahia Zedekiah Otieno akimkashifu Waruru ambaye sasa