Dumna yashangaza mashabiki wake

Muktasari:

Ofisa Mkuu wa FKF Pwani Kusini, Sumba Bwire alisema kutokana na Dumna kutofika uwanjani kwa mechi yao hiyo, Shells imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao mawili.

Kenya. Dumna FC iliwashangaza mashabiki wao wa nyumbani waliposhindwa kufika uwanja wao wa Msambweni kupambana na FC Shells kutoka Mombasa kwenye mechi ya Ligi ya FKF Pwani Kusini.
Ofisa Mkuu wa FKF Pwani Kusini, Sumba Bwire alisema kutokana na Dumna kutofika uwanjani kwa mechi yao hiyo, Shells imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao mawili.
“Ni sheria ambayo tunatumia kama timu haikufika uwanjani. Kwa sababu Dumna imeshindwa kucheza mchezo huo, tunatoa pointi tatu na mabao mawili kwa wapinzani wao wa FC Shells,” akasema Bwire.
Katika pambano lingine la ligi hiyo lilofanyika Uwanja wa Miritini World Bank, Miritini Combined ilishindwa kutamba uwanjani mwao kwa kuchabangwa bao 1-0 na Congo Boys ambayo imejizatiti kileleni mwa ligi hiyo.
Green Marine ya Ukunda ilijikuta taabani ilipotandikwa mabao 2-1 na Nyota ya Mombasa katika pambano lilofanyika uwanja wa Mzimuni hali Shanzu Swansea iliikamua Schalke 04 kwa kuilaza mabao 2-1 uwanjani Borstal.