Staa muziki Kenya kufuata nyendo za Profesa Jay

Friday July 21 2017

 

Mombasa, Kenya. Nyota wa muziki kutoka Mombasa anayetamba na ngoma yake mpya ‘Kichungu’,  Chikuzee ametangaza kufuata  nyayo za Profesa Jay na sasa katangaza kuwa anajiandaa kufunga ndoa na mchumba wake wa miaka mingi mwezi ujao.

Chikuzee ambaye baada ya kukaa kimya kwa miaka mitatu kutokana na bifu na Susumila, alirejea tena mwaka jana kwa kuaachia kazi kadhaa. Kwa sasa amesaini mkataba wa miaka mitano kufanya kazi na lebo ya mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Akizungumza kuhusu mipango yake, Chiku alisema anataka kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa miaka mingi kisha ataachie kazi kadhaa ambazo tayari zimetayarishwa Studio ya WBC jijini Dar es Salaam.