Kocha wa Harembee Stars ashusha presha

Wednesday November 8 2017

 

Rais wa Shirikisho la Soka  (FKF), Nick Mwendwa amesema hana mpango wa kumtimua kazi kocha wa timu ya Taifa Harambee Stars, Stanely Okumbi ambaye amekuwa akisisitiziwa aondoke kwa kukosa kuwa na mchango wa maana katika timu.
Tangu Kenya ilipotandikwa kwenye mechi mbili za kirafiki dhidi ya Iraq na Thailand, kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mashabiki na wadau mbalimbali ya kutaka kocha huyo atimuliwe kazi. Mwenyekiti wa makocha nchini kocha Robert Matano ni miongoni mwa wadau waliomkashifu Okumbi kwa kusema hana rekodi wala tajriba ya kuifunza Stars na ndio maana hata timu ‘ndogo’ zinazokamata nafasi ya chini mono kwenye msimamo wa FIFA, zinailaza Stars. “Aisee tusianze huo mjadala tena. Yaani nyie mwataka kutufanyia kazi yetu, mbona msituache tufanye kazi yetu. Hii timua timua ya makocha mumeizoea kiasi kwamba imekuwa ni kama mzaha sasa.”