Mwanamuziki Mercy Masika kamiminia sifa kibao mume

Muktasari:

 Masika kamtaja mumewe kuwa mwanaume wa shoka ambaye amechangia pakubwa ufanisi wake.

MWANAMUZIKI wa injili anayepepea kwa sasa Mercy Masika kamiminia sifa kibao mume wake David Muguro ambaye wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa.

 Masika kamtaja mumewe kuwa mwanaume wa shoka ambaye amechangia pakubwa ufanisi wake.

Mapema mwaka huu Masika alitibua kuwa mume wake huyo ndiye humpangia matumizi ya hela zake ili kumsaidia kueupuka ubadhirifu hasa uraibu wake mkubwa alionao wa kupenda kununua viatu.

 Akifunguka tena hivi majuzi, Masika alisifia uamuzi wake wa kukubalia kuposwa na jomba huyo ambaye anamwona kuwa muhimili mkubwa wa mafanikio yake kitaaluma kama mwalimu na mwanamuziki vile vile.

“Ndoa ni safari ndefu inayokuwa  katika mazingira yenye mapenzi, kujituma, heshima, mawasiliano, uvumilivu na kuaminiana. Kati ya maamuzi bora niliyowahi kufanya katika maisha yangu ni kumkubalia anipose na kisha kunifanya mke wake. Kanijenga sana” Masika alimsifia. Mumewe huyo amekuwa akiuysapoti muziki wake tangu alipoanza na hili lilithibitika kwenye tuzo za Groove Awards 207 alimsindikiza kupokea tuzo lake la Msanii bora wa kike wa Injili. Kwa sasa anafanya vyema na kazi yake ‘Shule Yako’  iliyotungwa na Pitson.