Modern Coast yapata ushindi bila jasho

Wednesday October 25 2017

 

By ABDULRAHMAN SHERIFF

MOMBASA. Modern Coast Rangers FC ilibahatika kupata ushindi bila ya kutoka jasho baada ya wapinzani wao wa GFE kushindwa kufika Uwanja wa Mbaraki Sports Club kucheza mechi ya Supaligi ya Taifa.
Katibu wa Modern Coast Rangers, Ferdinand Ogot alisema kutokana na kupata pointi hizo tatu za bwerere, wanaangazia mechi zao zilizobakia timu ishinde ili ifanikiwe kumaliza japo kwenye nane bora.
Kocha wa Mombasa Olympic, Joseph Oyoo aliwapongeza wachezaji wake baada ya kuilazimisha timu ya Makolanders FC sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Soka la Wanawake iliyofanyika Uwanja wa Camp Toyoyo jijini Nairobi.
Hata hivyo, matokeo hayo ya sare ya kufungana mabao 2-2 hata hivyo hayakumfurahisha kocha huyo aliyedai walikuwa watoke uwanjani wakiwa washindi kwani wapinzani wao walikomboa dakika za mwisho.
Oyoo alisema walistahili kushinda lakini bahati mbaya iliwafikia dakika za majeruhi wapinzani wao hao walipopata bao la kusawazisha. “Tuna imani kubwa ya timu yangu kufanya vizuri kwenye mechi zetu zilizobakia,” alisema Oyoo.