Bingwa wa Marathon Olimpiki 2016 atimuliwa miaka minne

Muktasari:

EPO (Erythropoietin) mojawepo ya madawa yaliyoharamishwa, hutumika sana mahospitalini kubusti utengenezaji wa seli nyekundu za damu mwilini ambazo husaidia sana katika usafirishaji wa Oxijeni mwilini.

NI aibu tu. Hii ni baada ya bingwa wa Marathon ya Olimpiki 2016 kule Rio De Janeiro, Brazil, Jemima Sumgong kupigwa marufuku ya miaka minne na Shirika la Kupambana na Pufya (ADAK), baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli EPO.
 Jemima 32, aliyeweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza Mkenya kushinda Marathon kwenye mashindano ya Olimpiki, sasa anaungana na rafiki yake Rita Jeptoo bingwa wa zamani wa Chicago na Boston Marathon 2014, anayehudumia marufuku ya miaka minne baada ya kupatikana na kosa sawia la matumiuzi ya EPO.
Ni dawa maarufu ambayo imehusishwa sana na wanariadha kadhaa waliopigwa marufuku.Sumgong alisimamishwa kushiriki shindano lolote Aprili mwaka huu na uchunguzi kuanzishwa mara moja, baada ya sampuli ya damu yake kupatikana ikiwa na chemchembe hizo za EPO. Akijitetea Sumgong alidai kuwa EPO hiyo iliingia mwilini mwake alipochomwa sindano na daktari mmoja katika hospitali ya Kenyatta Februari mwaka huu ili kuzuia uvujaji wa damu mwingi uliokuwa umesababishwa na kuharibika kwa ujauzito wake.