Lupita aibukia katika aksheni mwanzo mwisho Hollywood

Saturday June 24 2017

 

By THOMAS MATIKO

NYOTA mwigizaji wa Hollywood, Mkenya  Lupita Nyong’o,  kaibuka kwenye filamu mpya safari hii ikiwa ni ya aksheni  mwanzo mwisho.

 Katika filamu hiyo mpya ‘Black Panther’ itakayotoka Februari 2018. Filamu hiyo imekopa hadithi kutoka kwenye vilamu ya Captain America: Civil War.

 Kwenye sinema hiyo Lupita anaigiza kama Nakia, mpiganaji hatari wa kike wa jamii ya Wakanda aliyetwikwa majukumu yeye pamoja na wenzake wengine kulinda ufalme wa Wakanda dhidi ya maadui wanaowahangaisha.

 Kwa mujibu wa mapokezi ya ‘teaser’ ya filamu hiyo inayoandaliwa na kampuni ya Marvel, huenda ikawa filamu ya tatu kubwa  alizoshiriki Lupita tangu aliponusa ustaa 2012 kwenye filamu ya ‘12 Years a Slave’ iliyomwezesha kushinda Oscar.

 Filamu hiyo ilihusu unyanyasaji wa kiutumwa na ilimwezesha kupata michongo zaidi. Akizungumzia ujio wake huu mpya unaojiri baada yake kutokea kwenye filamu nyingine ya Star Wars: The Force Awakens alikoigiza kama Maz Kanata Lupita kasema. “Kuiona jinsi ile teaser ilivyotoka niliingiwa na mchecheto. Ni filamu nzuri hilo nawahakikisheini. Imenipa fursa ya kuonyesha uwezo wangu katika levo tofauti za kimaisha. Natamani sana ianze kuonyeshwa” Lupita aliiambia Access Hollywood siku chache zilizopita.   Pia Lupita alicheza kwenye filamu ya ‘Queen of Kwate’ iliyoshutiwa Uganda lakini haikuzua mshawasha sana.