Kenya yaishitaki Equatorial Guinea CAF

Muktasari:

Kenya na Equatorial Guinea zilikutana katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya  Afrika kwa wanawake (AWCON 2018). Katika mchezo huo, uliopigwa, Juni 6, ugani Kenyatta, mjini Machakos, Harambee Starlets ilishinda 2-1.

Nairobi. Shirikisho la Soka Kenya (FKF), imetuma malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Equatorial Guinea, ikilalamikia kitendo cha taifa hilo kutumia 'mamluki', wakati wa mchezo baina ya timu hizo mbili hivi karibuni.

Kenya na Equatorial Guinea zilikutana katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya  Afrika kwa wanawake (AWCON 2018). Katika mchezo huo, uliopigwa, Juni 6, ugani Kenyatta, mjini Machakos, Harambee Starlets ilishinda 2-1.

Kwa mujibu wa barua ya FKF, iliyosainiwa na Mkurugenzi wake Mkuu, Robert Muthoni kwenda kwa Equatorial Guinea iliwatumia wachezaji wawili 'mamluki' raia wa Cameroon. Wachezaji hao ni Celestine Basecu na Annette Msomo.

Kama madai ya Kenya yatathibitishwa, Equatorial Guinea, wanaweza wakakabiliwa na adhabu kali. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa taifa hili kushushiwa rungu la adhabu, baada ya FIFA kuwafungia katika michuano ya kusaka tiketi ya kwenda World Cup 2019, baada ya kuchezesha mamluki 10.