Brown Mauzo amkana live Akothee

Muktasari:

Brown Mauzo na Akothee wana historia ya toka zamani ambapo, waliwahi kuwa wapenzi licha ya mtanashati huyo kuendelea kukana kuwahi kutoka na mwanamama huyo tajiri mwenye watoto watano.

BAADA ya msanii Brown Mauzo kukana kuwahi kuwa mpenzi wa Akothee sasa kadai kuwa ni yeye ndiye aliyemtoa kimuziki.
Brown Mauzo na Akothee wana historia ya toka zamani ambapo, waliwahi kuwa wapenzi licha ya mtanashati huyo kuendelea kukana kuwahi kutoka na mwanamama huyo tajiri mwenye watoto watano.
Ushahidi wa picha yao ya kitambo wakilana denda iliyozagaa mtandaoni ni mojawepo tu ya thibitisho ingawaje Brown huwa mkali ishu iyo inapoibuliwa.
Pia, aliwahi kukiri kuwa wakati mmoja Akothee aliwahi kumnunulia gari ‘kishikaji’ lakini baadaye akampokonya. Tetesi zinaarifu kuwa Akothee alimpokonya gari hilo kwa sababu ya kupenda kuwazengua mademu wengine kwa kulitumia.
Huku pia kukiwa kumeibuka na tetesi mpya za kuwa bado wawili hao wanaonana kisiri siri na kwamba, Akothee ndiye anayegharamia maisha ya kifahari anayoishi kwa sasa Mauzo ikiwemo kufadhili kazi zake za muziki, mtanashati huyo kairuka stori hiyo.
Hivi majuzi akifunguka, Brown alikana kabisa kwamba kawahi kusaidiwa kivyovyote na Akothee kimuziki na badala yake kadai ni yeye ndiye kachangia muziki wa supastaa huyo wa kike.
“Akothee alichangia sana muziki wangu kama shabiki kwa sababu alikuwa anapenda kazi zangu ila hakuchangia mimi kusonga mbele. “Nimekuwepo tangu naanza kufanya muziki yeye akiwa bado. Nilikuwa mmoja wa niliomchukua, akaniambia anataka kuimba nikawa namwandikia mashairi na nikaweza kumwingiza kwenye game, ila hakuchangia kunisogeza,” amedai Brown Mauzo.