Ajabu, kweli Rayvany amefagiliwa

Saturday July 1 2017

 

By THOMAS MATIKO

SIO kawaida kwa wanamuziki kufagiliana wanapotia fora. Lakini ushindi wa juzi wa Rayvanny wa tuzo la BET International Viewers Choice, umemgusa rapa wa siku nyingi kutoka nyumbani Jua Cali  hadi akampongeza.

Akitiririka, Jua Cali, aliyeivaa jarida la Parents toleo la hivi majuzi pamoja na mkewe wa miaka minane, amemsifia msani huyo kutoka WCB, kwa kusema ushindi wake unaupa sifa muziki wa East Afrika kwa kuutangaza zaidi.

“Unajua ndoto yetu sisi wote ni kupeleka ngoma za East Afrika huko nje. Unajua mashindano yapo mengi sana, tunapigana na watu wa South Africa, West Africa, Marekani, watu wa Europe na wakati kuna msanii wetu anashinda tuzo kama hiyo, ni kitu kikubwa .

Kwa sababu sasa kinaweka East Afrika mahali pazuri hasa kwanza muziki kiswahili. Unajua mimi ni mtu wa wa Kiswahili so nikiona msanii anaimba kwa Kiswahili na ameshinda inapendeza sana.”

Kuhusu ujio wake mpya, Juacali  ambaye mapema mwaka juzi alitangaza kwamba atapunguza kasi za muziki ili kujishughulisha zaidi na uprodusa, kaahidi kuachia albamu yake ya nne Septemba mwaka huu aliyoiita ‘Mali ya Umma’.