Mshambuliaji Divock Origi wa Liverpool apaisha soka la Kenya

Thursday September 21 2017

 

By THOMAS MATIKO

MKONGWE wa soka kutoka Ujerumani, Lothar Mattheus, aliyepo nchini Kenya kwa siku kadhaa sasa kwa hisani ya Startimes ili kuitangaza Ligi Kuu Kenya, ameshusha sifa kibao kwa straika wa Liverpool, Divock Origi, mwenye asili ya taifa hili.
Mattheus aliyestaafu soka la ushindani mwaka 2000 baada ya kupiga nafasi za kiungo na beki katika klabu za Bayern Munich na Inter Milan, yupo nchini akifanya kiliniki za soka ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuusongesha mbele mchezo huo nchini.
Mattheus anayekiri kutokuwa na ufahamu mkubwa wa soka la Kenya, lakini anakiri kuwapo kwa vipaji kama vya Origi, ni uthibitisho tosha kwamba taifa hili lina talanta za kutosha ila kinachokosekana na mipango ya kuziimarisha.
“Nimegundua hapa hamna makocha wazuri na miundo misingi, ndio sababu mapenzi yenu kwenye soka yanakwenda na maji. Kumwona mchezaji kama Origi aliyeichezea Ubelgiji mara 22 akiwa na asili ya Kenya, ni ithibati tosha mna vipaji si haba,” Mattheus katiririka.