Burudani

Walishtuka kijanja mapema

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

DULLY SYKES 

By THOMAS NG’ITU  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Ijumaa,Februari3  2017  saa 13:57 PM

Kwa ufupi;-

  • Mwanaspoti inakuletea orodha ya waimbaji wa muziki wa kizazi kipya nchini ambao waliona fursa mapema na kuamua kufungua studio na sasa wanakula maisha kilaini

KUNA baadhi ya wasanii wajanja sana. Licha ya kufanya vema kwenye fani huwa wanajisongesha kimtindo kwa kutambua kuwa wakati ukuta.

Uzoefu wanaokuwa nao kwenye fani, huwapa nafasi ya kuchangamkia fursa ya kuwa watayarishaji wa muziki, hivyo kujikuta hata kama kazi yake ya uimbaji itabuma, hawezi kupata stress kwa vile hupiga hela ndefu kama kawaida.

Mwanaspoti inakuletea orodha ya waimbaji wa muziki wa kizazi kipya nchini ambao waliona fursa mapema na kuamua kufungua studio na sasa wanakula maisha kilaini, hata kama shoo zimewakataa kutokana na ushindani uliopo ama umri kusogea.

Prince Dully Sykes

Msanii huyu mkongwe aliyetamba na nyimbo zake kali kinoma kwa wakati huo na mara nyingi kazi zake alikuwa akizitengeneza kwa Prodyuza Mika Mwamba, aliyekuwa akichuana miaka hiyo na wakali kama P. Funk na Master Jay wa MJ Records.

Dully baada ya kujishtukia kuwa umri unampa kisogo na asipokuwa makini atakuja kuchekwa, fasta alifungua studio inayofanya vema kwa sasa nchini.

Mkali huyo anamiliki studio hiyo ya 4.12 ambayo imefanya kazi nzuri sana kama Run Dsm ya P the Mc ambayo ndani yake kuna msanii Young Killer na Dully mwenyewe, lakini vile vile hata Na mimi nayo imefanywa katika studio hizo. Kitu cha kufurahisha ni kwamba, nyimbo zote za sasa za Dully amekuwa akijitengenezea mwenyewe hivi sasa hiki ni kipaji ambacho inawezekana amekipata kutokana na kutembea kwa watayarishaji wengi wakubwa.

Sir Juma Nature

Mkali huyu mwingine maarufu kama Kibla ni kati ya wasanii wachache ambao walikuwa wanakubalika kwa mtayarishaji mtata P Funk Majani. Sir Nature ngoma zake zote za zamani zilikuwa zina mdundo mzito kutoka studio za Bongo Record kama ile ngoma ya Ugali, Sitaki Demu na Hakuna Kulala.

Lakini, baada ya kupishana kauli na kuunda kundi lake la Wanaume Halisi aliamua pia kufungua studio ya Halisi Records ambayo alifanya ngoma zake kadhaa.  Licha ya kumiliki studio, lakini bado aliendelea kurudi kwa Majani kwani mjanja wake na kutoa ngoma kama ‘Dogo’ ambayo ilibamba kinoma.

Quick Rocka

Quick ni kichwa kutoka katika kundi la Rockers Family, jamaa katamba na ngoma zake kadhaa, lakini baadaye akausoma upepo na kuona kuwa kama atachelewa sana akitegemea kuimba peke yake itakula kwake, hivyo akaanzisha studio zake.

1 | 2 Next Page»