Mademu wa mastaa Arsenal,Chelsea tishio

Saturday January 28 2017

 

By Thomas Matiko

WIKENDI hii Ligi Kuu ya England ambayo kwa sasa inasisimua vilivyo, inasimama kidogo, kupisha Kombe la FA.

Achana na Kombe la FA twendwe kwenye kazi yenyewe. Ukweli ni kwamba kuna timu sita zimekabana shingo. Hizo zote zinawania kama si ubingwa basi nne bora na utamu ni kwamba timu hizo zina makocha wanaoaminiwa kuwa bora duniani.

Mpaka sasa mechi 22 zimeshapigwa huku Chelsea wakiwa juu kwa pointi 55 nafasi ya pili imejikita Arsenal ambayo imezidiwa pointi nane. Lakini Kama hujui, habari ni kwamba Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametangaza vita takatifu, amesema lazima awakimbize vinara wanaonolewa na Kocha Antonio Conte.

Wakati ushindani ukiendelea uwanjani, huku nyumbani pia kuna sarakasi za kuwasukuma wanaume wa shoka katika vita kubwa ambayo itaishia pale Mei mwaka huu. Hapa tunazungumzia wanawake wa mastaa wa klabu za Chelsea na Arsenal.

Makala haya yanawaweka mezani mademu wa ‘First 11’ ya timu hizo. Mademu hao pia watashuhudia shughuli kubwa kati ya Chelsea Arsenal Februari 4, yaani ni mwendo wa Jumamosi ijayo tu.

ARSENAL (4-2-3-1)

Martina (Petr Cech)

Martina ambaye alifunga pingu za maisha na kipa huyu 2003, amekuwa akimpa sapoti mumewe nje na ndani ya uwanja. Itakumbukwa Desemba 14, 2015, Cech alipoifikia rekodi ya EPL ya kipa aliyecheza mechi nyingi kwenye ligi hiyo bila kufungwa katika historia, iliyowekwa na kipa mstaafu David James, Martina alimwandalia keki spesho yenye nembo ya tisheti ya Fly Emirates na namba 169. Kusherehekea hatua hiyo katika taaluma yake. Ilikuwa ni kwenye mechi dhidi ya Aston Villa ambayo Cech alifikisha mechi 169 katika Ligi ya EPL bila ya kufungwa bao (Clean Sheet) na kuweza kuifikia rekodi ya miaka mingi ya James. Ingawa Martina ni msiri sana, akipendelea maisha ya kimya kimya, sapoti kwa mume wake kila anapokuwa uwanjani huwa katika levo tofauti kabisa.

Isabel Ramos (Nacho)

Isabel ni mke wa beki wa kushoto anayeunda kikosi cha kwanza cha mzee Wenger. Isabel si shabiki sugu wa soka na itakumbukwa mwaka 2014, alishambuliwa na shabiki mmoja wa Arsenal kwa kuwa na idadi ndogo ya mashabiki kwenye Twitter ambapo kwa kawaida wanawake wa wachezaji huwa na wafuasi wa kutosha kutokana na sifa za wapenzi wao.

Claire (Laurent Koscielny)

Ni demu wa siku nyingi wa kapteni msaidizi wa Arsenal Koscielny na walifunga ndoa 2015. Demu huyu ni shabiki namba moja wa beki Koscielny akiwa na mazoea ya kuhudhuria mechi za Arsenal kumpa morali mumewe.

Kwenye Euro 2016, ambayo Ufaransa, ilifika fainali, Claire alijumuika na wenzake kuvalia jezi za Ufaransa zenye majina na namba za wapenzi wao na kuwashabikia kinoma.

Vjosa Kaba (Shkodran Mustafi)

Mustafi alitua Arsenal mwaka jana kupiga jeki safu ya kati ya ulinzi na ameishia kuwa nguzo muhimu wa kikosi cha kwanza cha Wenger.

Kabla hajahamia Uingereza, alimuoa kimya kimya demu wake Vjosa ambaye ni msiri sana sawa na mpenziwe ambao ni wafuasi wakubwa wa dini ya Kiislamu. Licha ya kuwa haonekana uwanjani sana, Vjosa huandamana na Mustafi kwenye hafla nyingi za kispoti .

Berta Requeno (Bellerin)

Berta ni mpenzi wa beki wa kulia wa Arsenal na miongoni mwa wanawake wanaotoa sapoti kubwa kwa wapenzi wao nje na ndani ya uwanja. Berta huhudhuria na kutazama kila mechi ya Arsenal, sapoti ambayo imemfanya Bellerin kuchapisha majina yake kwenye buti zake za mchezo.

Collen Rowlands (Aaron Ramsey)

Collen amekuwa ubavuni mwa kiungo mkabaji Ramsey kwa miaka kadha sasa. Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka miwili sasa tangu walipooana na wamejaliwa mtoto. Licha ya Collen kuwa mwanamke msiri sana, sapoti yake kwa mumewe ambaye amekuwa Arsenal kwa miaka nane haifichiki. Mara kadhaa ameonekana akitangaza jezi na mpira ya Arsenal kwenye matangazo mbalimbali na inathibisha mchango wake katika gemu ya mumewe.

Leonita Lekaj (Granit Xhaka)

Ndiye demu wa kiungo fundi mwenzake Ramsey ambaye pia humtia morali. Lekaj ana wafuasi zaidi ya 39,000 kwenye Instagramu na mara nyingi kadhaa ameitumiwa kumpigia debe mpenziwe anapokuwa mchezoni.

Melaine Slade (Theo Walcott)

Melaine ni msiri kupita maelezo na tofauti na wenzake, hana mazoea ya kuandamana na mumewe, ambaye ni mpenzi wake tangu shule ya msingi, katika kila hafla anayoalikwa. Hata hivyo akiwa ni mtaalamu wa masuala ya michezo inayohusu misuli na majeraha amekuwa nguzo muhimu.

Mandy Capristo (Mesut Ozil)

Mandy na Ozil wanaishi kwenye mapenzi ya kutesana, wakitemana na kurudiana. Mrembo huyo humpa sapoti kwa asilimia 100, Ozil kimchezo nje au ndani. Amekuwa akiachana na kazi yake ili kumfuata Ozili katika kila klabu alinayochezea kumpa sapoti.

Lai Grassi (Alex Sanchez)

Mrembo huyu amekuwa akimsapoti winga machachari Sanchez kwa kuvalia jezi ya Arsenal yenye maandishi ‘I Am a Gunner’ katika kila mechi anayohudhuria.

Jennifer Giroud (Giroud)

Amekuwa msaada mkubwa wa Giroud kwani licha ya hata kufanyiwa mchepuko naye miaka miwili iliyopita, Jennifer alisamehe. Licha ya kuwa ni msiri sana, hakuna mechi aliyopangwa mumewe ambayo yeye hukosekana.

CHELSEA: 4-2-3-1

Marta Dominguez (Thibaut Courtois)

Marta ndiye demu wa kipa huyu nambari wani wa Chelsea na mara kwa mara amekuwa akihudhuria mechi za The Blues kumshabikia mpenzi wake. Hata Courtois anapokuwa hachezi, Marta bado hukata tiketi kucheki mechi ya klabu ya mpenzi wake ambaye wamebahatika mtoto mmoja.

Adriana Azpilicueta (Cesar Azpilicueta)

Adriana ni mke wa beki kulia Azpilicueta na ijapokuwa hahudhurii mechi nyingi za Chelsea, kutokana na kuwa msiri sana na maisha yao, anasemekana kuwa mdau mkubwa anayempa msukumo wa uwanjani mlinzi huyu.

Marcos Alonso

Beki huyu wa kushoto hajajua mapenzi lakini kitu kinachompa motisha ni familia yake, ikiwa ni pamoja na dada zake.

Gemma Acton (Gary Cahill)

Gemma ndiye mke wa beki matata Cahill ambaye amekuwa katika ubora wake. Katika kumpa sapoti ya uwanjani, Gemma anaamini kuwa ubora wa Cahill unaoonekana umechangiwa na ndoa yao.

Sara Madeira (David Luiz)

Sarah ni mpenzi wa beki Luiz, ambaye tangu arejee Chelsea amechangia udhibiti wa ngome ya ulinzi wa timu. Wamekuwa wapenzi kwa miaka zaidi ya mitano sasa tangu akiwa Benfica na licha ya kuwa mwanafunzi, hujitahidi sana kutokea kwenye gemu za mpenzi wake.

Ngolo Kante

Kiungo huyu mpole hana muda na mademu na familia yake ndiyo impayo sapoti kubwa uwanjani.

Aleksandra Matic (Nemanja matic)

Aleksandra ni mke nyumbani ambaye amekuwa akimfuata mumewe kutoka taifa moja hadi nyingine anaposajiliwa kucheza, wakiwa tayari wameishi kwenye nchi tano.

Vanessa Martins (WIllian)

Vanessa ambaye ni wakili alikutana na Wilian Sao Paulo, Brazil na kisha akaamua kuachana na kazi yake na kujiunga na winga huyo Ukraine kumpa sapoti ya uwanjani, kabla yao kuhamia tena London 2013. Wana watoto wawili mabinti na walioana 2011.

Victor Moses

Winga huyu ni msiri sana na hajawahi kumweka hadharani wala kumtaja jina demu wake ambaye kamzalia watoto wawili. Wanaamini zaidi katika kulinda uhusiano wao kwa kuifanya siri ili pia kumwezesha Moses azingatie soka zaidi.

Natasha (Eden Hazard)

Ni muhimili wa ndoa yao akiwa ni mke nyumbani ambaye mchango wake mkubwa kwa Hazard ni kuangalilia watoto wao wawili na kutoa faraja kwa Hazard nje na ndani ya uwanjani.

Diego Costa

Kinara huyu wa mabao wa Chelsea kwa sasa naye hana demu tangu kutemwa na kimwana Michele Zuanne kwa kujaribu kumtongoza dada yake.​

Benchi la Chelsea

John Terry ambaye amefunga ndoa na mwanadada Toni na Fabregas ambaye ni mume wa mwanadada Daniella.