Jamani Tonto Dike hajui Kiingereza

Tonto Dike

Muktasari:

Imekuwa ni jambo la kawaida kuona watumiaji wa mitandao kama Twitter, Facebook na mingineyo kutumia maneno ya Kiingereza kwa kifupi wakiwakilisha ujumbe fulani kwa jamii.

WATU wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii, kuboresha uwezo wao wa kuongea hususani lugha wanazozitumia.

Imekuwa ni jambo la kawaida kuona watumiaji wa mitandao kama Twitter, Facebook na mingineyo kutumia maneno ya Kiingereza kwa kifupi wakiwakilisha ujumbe fulani kwa jamii.

Tonto Dikeh naye akiwa mmoja wa watumiaji wa mitandao hiyo, amekuwa akitumia njia hiyo. Lakini tofauti na matarajio yake, mara nyingi amekuwa akikosolewa na wafuasi wake wanaodai kwamba anachoandika huwa hakieleweki.

“Hili nimeliona na ninakiri kuwa sina ujuzi wa kutosha katika kuwasiliana hususani katika lugha ya Kiingereza. Hivyo naahidi kurudi shule kwa ajili ya kunoa Kiingereza changu,” aliliambia gazeti la Vanguard.

“Mnataka nirekebishe uandishi wa Kiingereza changu? Hamna shida nitajitahidi kufanya hivyo.”

Cha kuchekesha zaidi ni hata pale alipoandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Facebook pia aliukosea.