Waigizaji wanaoongoza kwa kashfa Nollywood

KWA namna moja au nyingine imekuwa vigumu kwa muigizaji wa kike wa Nollywood kukwepa kutuhumwa kwa kashfa mbalimbali.

Kila mmoja kwa wakati wake amekuwa akitumia njia anayoifahamu kukabiliana na kashfa hizo. Wako wanaoamua kwenda mahakamani, wengine huchukua sheria mkononi kwa kupambana na wanahabari walioibua kashfa hizo na wengine huamua kunyamaza kimya.

Ifuatayo ni orodha ya waigizaji wa kike wa Nollywood ambao wamekuwa wakikashifiwa mara kwa mara.

Kinachofurahisha zaidi ni kashfa hizi ziwe za ukweli au uwongo, hazikuweza kuathiri kazi zao na badala yake zimewaimarisha na kuwafanya wawe juu zaidi na kujizolea mashabiki lukuki.

 

Tonto Dikeh

Tonto anatajwa kuwa kiongozi katika kundi hili, ni mara chache sana unaweza kulikosa jina lake kwenye vichwa vya habari vya machapisho mbalimbali nchini Nigeria.

Katika habari kumi zinazoandikwa kuhusu mwigizaji huyu, saba kati ya hizo ni kashfa. Inasadikiwa kuwa nyingi kati ya kashfa anazotuhumiwa nazo ni za ukweli.

Na hii ni kutokana na ukweli kwamba amekuwa msanii mwenye tabia tofauti kidogo, kwani ni jambo la kawaida kwake kufanya mambo hata yale yasiyokuwa ya kawaida katika jamii.

Kwa mfano hivi karibuni ameigiza filamu ambazo zimeweka sehemu kubwa ya mwili wake wazi. Kitendo ambacho kinapingwa na wengi nchini Nigeria.

Si hivyo tu amekuwa na tetesi za kujihusisha kimapenzi na wasanii kibao nchini humo wakiwamo Tuface, KC Presh, Wizkid na Iyanya.

 

Nuella Njubigbo

‘Ella’ kama mashabiki wanavyomuita amekuwa akihusishwa na hadithi kadhaa za  mapenzi ndani na nje ya tasnia ya filamu nchini Nigeria.

Hadithi ya kwanza ilikuwa ni ile ya kujihusisha na mapenzi na Yul Edochieb ambayo ilionekana ina ukweli ndani yake.

Baada ya kuenea kwa kashfa hiyo, Ella alijitokeza hadharani na kupinga . Lakini kama ilivyo kwa msemo wa waswahili jasiri haachi asili, muda mfupi baadaye iliibuliwa kashfa yake nyingine ya mapenzi  kati yake na muongozaji filamu, Tchidi Chikere.

Licha ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari akipinga uvumi huo, muda si mrefu iliripotiwa kuwa alikuwa na mahusiano na gavana wa jimbo moja nchini Nigeria.

Wengine wanaotajwa kuwahi kuwa na mahusiano naye ni pamoja na mwanasoka Emmanuel Emenike na wengine kibao.

 

Cossy Orjiakor

Cossy ni miongoni mwa mastaa wapole sana katika tasnia ya burudani Nollywood. Lakini huo haukuwa mwamvuli wa kujificha kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Namna anavyoachia wazi sehemu kubwa ya maziwa yake inatosha kabisa kumuelezea na wakati mwingine ndio kimekuwa chanzo cha watu wanaomtazama kukubaliana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Kashfa maarufu inayomkabili mrembo huyu ni ile ya kulipwa kwa ajili ya kulala na mbwa. Licha ya kuipinga vikali lakini hadi leo hii wako wasiokubaliana naye.

Hivi karibuni aliweka picha zake za utupu kwenye ukurasa wake wa Tweeter na pia aliweka picha alizopiga zikionyesha nguo yake ya ndani.

 

Lola Alao

Hivi karibuni ugomvi uliomhusisha rafiki yake wa karibu Bisi Ibidapo-Obe na mbunge mmoja Dino Melaye. Ugomvi huo ulikuwa ni wa mapenzi, Lola alisema alituhumiwa visivyo.

Kabla ya mtafaruku huo wa kwanza Lola aliwahi kupatwa na kashfa ya uchawi iliyobainishwa na mume wake wa zamani, ambayo ilipamba vichwa kadhaa vya magazieti.

Katika mahojiano yake na kituo kimoja cha televisheni, Lola alikataa kulizungumzia hilo na badala yake alibakia kumsifia mume wake huyo na kusema:  “Alikuwa mwanaume mzuri licha ya kuvunjika kwa ndoa yetu.”

 

Funke Akindele

Funke anatajwa kuwa staa mwenye kashfa nyingi za mapenzi. Inaelezwa kuwa amewahi kuwa na mahusiano na wanaume kadhaa maarufu nchini humo kabla ya kufunga ndoa na Alhaji Kehinde Almaroof Oloyede.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali  vya habari, muigizaji huyo licha ya kuwa kwenye ndoa, bado amekuwa na mahusiano ya siri na wanaume wengine mbali ya mume wake.

 

 

Genevieve Nnaji

Licha ya usupastaa aliokuwa nao katika tasnia ya burudani kitaifa na kimataifa, vichwa vya habari vinavyomtaja Genevieve vimekuwa vikionekana mara kwa mara katika magazeti na vyombo vingine vya habari, vikiongozwa na kashfa anazotuhumiwa nazo.

Kabla ya staa huyu kufikia kwenye daraja alilonalo leo hii imewahi kuripotiwa kuwa amekuwa akijihusisha kimapenzi na watu tofauti tofauti wakiwamo waigizaji wenzake kama Pat Attah, Kunle Coker na wengine kibao.

Kubwa zaidi ni pale anapotajwa kuwa aliwahi kuwa na uhusiano na makamu wa rais wa zamani. Kwa sasa inaelezwa kuwa anatoka na  mwanamuziki D’Banj.

 

Faithia Balogun

Aliwahi kuwa mke wa nguli wa uigizaji Nollywood, Saidi Balogun. Lakini hili halikumfanya asifuatiliwe na hata kumtuhumu kwa kashfa tofauti tofauti.

Awali iliripotiwa kuwa aliwahi kupigana na mwigizaji mwenzie eti kwa kuwa alikuwa na mahusiano na mwanasiasa Rotimi Ajanaku ambaye alikuwa akitoka na yeye.

Pia aliwahi kuripotiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mkurugenzi mmoja huko Nollywood.

Mbali na hayo anatajwa kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa ya kigogo mmoja nchini humo.