Makala

Irene sasa ameamua kabisa aisee

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

Irene Paul 

By new  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Jumanne,Aprili16  2013  saa 24:0 AM

MWIGIZAJI, Irene Paul, amedai kuachana na kazi ya utangazaji baada ya kubaini filamu inamlipa zaidi na kumpa fursa ya kufanya mambo makubwa. ìKwangu mimi filamu inanilipa, ndiyo maana nimeachana na kazi nyingine zote ili niwe makini na kazi ya uigizaji. Hapa ninayaona maslahi moja kwa moja," alisema. "Pia filamu imenikutanisha na watu mbalimbali, pia imebadilisha maisha yangu napata ninachohitaji bila wasi wasi." Irene aliyewahi kufanya kazi na vituo vya luninga vya C2C na Clouds TV vya Dar es Salaam alipewa nafasi na Ray kwenye uigizaji na kufanya vizuri. Msanii huyo ameshiriki filamu na wakongwe katika tasnia wakiwamo Steven Kanumba (marehemu sasa). Filamu alizoigiza ni 'I Hate My Birthday', 'Kibajaji', 'More Than Pain' na 'Kalunde' aliyoitengeneza mwenyewe.


Makala

Jamani! Mariam wala hataki skendo

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

Mariam Ismail 

By new  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Jumanne,Aprili16  2013  saa 24:0 AM

MARIAM Ismail amedai kuwa hahitaji skendo ili kujiongezea umaarufu kama wanavyofanya wasanii wenzake wa Bongo. "Binafsi sihitaji skendo ili niwe maarufu bali ninachofahamu ni uwajibikaji katika kazi ninayopewa na mtayarishaji wa filamu husika, ninachohitaji ni kusoma muongozo (script) vizuri kisha kuvaa uhusika kulingana na nafasi nitakayopewa kuigiza," alisema. "Mara nyingi wasanii tunahitaji hisia, hicho ndicho ninachofanya katika filamu zote nilizoigiza na kunifanya niwe bora." Msanii huyo ameshiriki katika filamu kadhaa zikiwamo 'Best Man', 'Wrong Decision', 'Identical', 'Samatha' na 'Doa La Ndoa'. Msanii huyo ni matunda ya kazi ya Mtitu kutoka 5 Effect ambaye mara nyingi hukuza vipaji vya filamu Bongo, makali ya Mariam yanafananishwa na ya mwigizaji wa kike wa Nigeria, Omotola Jalade.


Makala

Lulu hata hajielewi kabisa

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

Lulu 

Lulu 

By new  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Jumanne,Aprili16  2013  saa 24:0 AM

MSANII wa filamu, Lulu, ametamka kwamba hakuwahi kufikiria kwamba kwenye maisha yake atakumbana na majaribu makubwa kama anayopitia kwa sasa. Msanii huyo hivi karibuni aliachiwa kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili akituhumiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii maarufu, Steven Kanumba. Lulu alikuwa katika simanzi kubwa wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Kanumba iliyofanyika jijini Dar es Salaam na alishindwa hata kuzungumza kwa kirefu. Msanii huyo alionekana mwenye mawazo na anayekumbuka vitu vingi kuhusu marehemu. ìSikuwahi kufikiria hata siku moja kama naweza kupitia katika mapito kama haya,î alisema Lulu huku akilia kwa uchungu. Kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha Kanumba kitokee ilifanyika katika Kanisa la KKKT Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita kwa ibada kisha wasanii kushiriki katika chakula cha mchana kabla ya kuelekea makaburini na baadaye kuhamishia shughuli hizo viwanja vya Leaders.