Zlatan bora kuliko Messi, Ronaldo

Tuesday November 12 2013

 

PARIS, UFARANSA

BEKI wa Paris Saint-Germain, Thiago Silva, amerudia maneno ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, akiamini kwamba kwa sasa mshambuliaji wa PSG, Zlatan Ibrahimovic, ni zaidi ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Mara baada ya Zlatan kuifunga Anderlecht ya Ubelgiji mabao manne katika pambano la Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki chache zilizopita, Wenger alikaririwa akisema kwamba staa huyo wa Sweden ni bora kuliko Messi na Ronaldo. Lakini sasa, Silva naye anatilia mkazo maneno hayo.

“Kama shabiki wa soka nampenda Ibrahimovic. Nina uhakika atakuwa katika wachezaji watatu bora watakaowania taji la Mwanasoka Bora wa Dunia. Itakuwa ngumu kwake kushinda, lakini nadhani anastahili. Kwa sasa anacheza vizuri kuliko Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.”

Jumamosi Zlatan aliiongoza PSG kutanua pengo lake la uongozi kwa pointi nne dhidi ya Lille baada ya kuichapa Nice mabao 3-1 nyumbani.