Zidane: Siwahofii Bayern Munich

Saturday March 18 2017

 

Madrid, Hispania. Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema mechi kubwa iliyopo mbele yao dhidi ya Buyern Munich, robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wachezaji wake hawana haja ya kuwa na hofu kwa kuwa aliyatarajia hayo kutokea wakati wa kupanga ratiba.

Zidane ambaye amewahi kufanya kazi na Kocha wa Buyern Munich akiwa msaidizi wake akiwa Los Blancos, amesema wachezaji wake wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mechi hizo.

Tangu amekuwa na kikosi hicho cha Santiago Bernabeu, ameiwezesha timu yake kuibuka na mataji msimu uliopita.