Spoti Majuu

Wenger ataka Ozil afunge

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Jumanne,Februari14  2017  saa 15:38 PM

Kwa ufupi;-

Kocha huyo wa Arsenal ameamua kumchenjia staa huyo wa Ujerumani aliyemsajili kwa pesa nyingi sana Pauni 42.5 milioni kwamba abadilike na aonyeshe kiwango bora tena kuanzia kwenye mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich kesho Jumatano.

ARSENE Wenger ameanza kung’aka kuhusu kiwango kibuvu cha supastaa wake anayegomea kusaini mkataba mpya, Mesut Ozil.

Kocha huyo wa Arsenal ameamua kumchenjia staa huyo wa Ujerumani aliyemsajili kwa pesa nyingi sana Pauni 42.5 milioni kwamba abadilike na aonyeshe kiwango bora tena kuanzia kwenye mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich kesho Jumatano.

Ozil amekuwa hafungi na jambo hilo linamfanya Wenger ambadilikie na kumtaka aanze kufunga kama kweli anahitaji mkataba mpya unaostahili.

Wenger alisema: “Pengine kimekuja sasa kipindi cha Mesut kuanza kufunga tena. Anapaswa kufanya hivyo. Anakosa sana nafasi ambazo hakika anapaswa kufunga. Nakubali kwamba hajiamini na hilo ni kwa sababu yetu tunaamini kuna kitu spesho cha zaidi ambacho atafanya.”

Ozil (28), hajafunga bao lolote kwa kipindi cha miezi miwili sasa huku kikosi chake cha Arsenal kikiondolewa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Ozil amegoma kusaini dili mpya akidai kwamba hawezi kufanya hivyo hadi hapo atakapofahamu kuhusu hatima ya baadaye kama Wenger ataendelea kuwa kocha kwenye kikosi hicho hadi msimu ujao.

Ozil alishambuliwa sana kwa kiwango chake cha ovyo wakati walipochapwa 3-1 na Chelsea wiki iliyopita.