Pique asema hakuna wa kumfunika Messi

Monday March 20 2017

 

Barcelona, Hispania. Beki wa Barcelona, Pique amesema kwamba mafanikio aliyoyapata mchezaji mwenzake, Lionel Messi kamwe hayatakuja kujirudia kwenye klabu hiyo.

Messi ameifungia timu yake mabao muhimu wakati ikiipa presha Real Madrid. Barca iliibuka na ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Valencia na kujiimarisha kwenye msimamo wa La Liga wakiwa nyuma kwa Madrid kwa tofauti ya pointi mbili.

Raia huyo wa Argentina mwenye miaka 29, anaongoza kwa ufungaji wa mabao  kwenye La Liga baada ya kutupia jumla ya mabao 25.

“Tunamtarajia mchezaji bora wa kihistoria,” alisema Pique kupitia tovuti ya klbau hiyo.