Mourinho aisikitikia Man City

London, England. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema amehuzunishwa kitendo cha kutolewa Manchester City katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kikosi hicho cha Pep Guardiola kilikwama kwenye hatua ya 16 bora baada ya  mchezo wake wa awali  kushinda kwa mabao 3-1 lakini mchezo wa marudiano ikalala kwa mabao 2-0 na kufanya timu hizo kuwa na mabao sawa 6-6 lakini Monaco ikapata mwanya wa kupenya hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Katika timu zilizopo kwenye kwenye Ligi Kuu ya England, ni Manchester United na Leicester City ambazo zimebaki kwenye uwakilishi wa mashindano ya Ulaya.

Mourinho alisema kufungwa Manchester City na kuondolewa kwenye mashindano hayo kumemuhuzunisha  na kumewapa wakati mgumu Manchester United kupambana kuingia kwenye nafasi nne za juu katika mashindano hayo.

“Nimekosa raha kutolewa Manchester City. Sifanyi utani katika jambo hilo. Ni jambo baya kwetu kwa sababu kuna sababu nyingi zinazotufanya kuhuzunika kuhusu jambo hilo,”aliiambia BT Sport.

“Ni jambo baya kwetu kama timu kutoka England siyo jambo la kufurahia hasa kwa timu ambazo tupo nafasi ya juu kukosa mwakilisho katika mashindano hayo” Watakuwa wakicheza mechi moja kwa wiki kama ilivyokuwa mwanzo wa msimu huu”

Tunajua ugumu tutakaokuatana nao kwenye hatua ya robo fainali ya mashindano hayo. Tutapambana kwa kadiri ya uwezo wetu”

Mourinho amehuzunishwa kuhusu ratiba inayoikabili Manchester United Baada ya ushindi wake wa bao 1-0 juzi dhidi ya Rostov huku akiwa na maumivu baada ya kutolewa na Chelsea katika Kombe la FA. Hivyo kesho atakuwa na kibarua kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Middlesbrough.