Mourinho afunguka tena kuhusu Pogba

Muktasari:

Kiungo huyo Mfaransa alirejea Man United akitokea Juventus kwa uhamisho wa Pauni 89 milioni ikiwa ni miaka minne tu kupita tangu alipoondoka Old Trafford kwenda kujiunga na miamba hiyo ya Italia.

JOSE Mourinho amewataka watu waache kumwaandama sana Paul Pogba kutokana na uhamisho wake wa pesa nyingi klabuni Manchester United.

Kiungo huyo Mfaransa alirejea Man United akitokea Juventus kwa uhamisho wa Pauni 89 milioni ikiwa ni miaka minne tu kupita tangu alipoondoka Old Trafford kwenda kujiunga na miamba hiyo ya Italia.

Pogba bado hajaanza kuonyesha kiwango kilichotarajiwa na wengi, lakini Mourinho amewaambia watu, staa huyo ana kipaji kikubwa na anachopaswa kufanyiwa ni kuaminiwa na kupewa muda kuzoea mazingira ambayo aliachana nayo miaka minne iliyopita.

“Pogba anaweza kucheza nafasi nyingi sana uwanjani. Tatizo si nafasi, tatizo ni mfumo. Hilo ndilo ninaloliona kwa upande wangu, ametokea kwenye timu inayocheza staili tofauti, hivyo anahitaji nafasi kujiweka sawa, hasa kwa mchezaji anayecheza kiungo.

“Nadhani kila mtu anafahamu ugumu wa kuzoea mazingira ya kiuchezaji na hali ya hewa kwa haraka. Pogba bado ana umri mdogo wa kumfanya arudi kwenye makali yake, kisha mtaanza kumfurahia kwa namna atakavyorejea kwenye kiwango chake cha juu kabisa,” alisema Mourinho