Man United mbabe wa Man City

File Photo

Muktasari:

Baada ya kuchapwa bao nne bila kwenye mechi iliyopita ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea, Man United chini ya kocha, Jose Mourinho ilihamishia hasira kwa mahasimu wao wa Jiji la Manchester na kuibuka kidedea kwenye Manchester derby kwa ushindi wa bao 1-0.

London, England. Manchester United haitaki tena ujinga, baada ya jana usiku kushusha kipigo kwa mahasimu wao Manchester City katika mchezo wa Kombe la Ligi uliofanyika Uwanja wa Old Trafford.

Baada ya kuchapwa bao nne bila kwenye mechi iliyopita ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea, Man United chini ya kocha, Jose Mourinho ilihamishia hasira kwa mahasimu wao wa Jiji la Manchester na kuibuka kidedea kwenye Manchester derby kwa ushindi wa bao 1-0.

Bao la kipindi cha pili kutoka kwa Juan Mata lilitosha kupeleka kilio kwa kocha, Pep Guardiola ambaye sasa ameshuhudia mchezo wa sita timu yake ikicheza bila ya ushindi. Mata alifunga bao hilo dakika ya 54 baada ya kumalizia pasi ya Zlatan Ibrahimovic.