Mahrez awaongoza kina Mane kwa mabao

 Sadio Mane

Muktasari:

Pierre -Emerick Aubameyang alikuwa staa wa kwanza kutikisa wavu wakati Gabon ilipotoka sare bao 1-1 na Guines-Bissau, lakini Riyad Mahrez akaja kujibu kwenye mechi ya sare ya mabao 2-2 na Zimbabwe kwa kupiga mbili, kabla ya supastaa mwingine wa nguvu Afrika, Sadio Mane naye kutupia wavuni wakati Senegal ilipoichapa Tunisia 2-0.

MASTAA wa Afrika wameanza kuonyesha cheche zao kwenye michuano ya Afcon 2017 kutokana na kushindana kwenye kupasia nyavu.

Pierre -Emerick Aubameyang alikuwa staa wa kwanza kutikisa wavu wakati Gabon ilipotoka sare bao 1-1 na Guines-Bissau, lakini Riyad Mahrez akaja kujibu kwenye mechi ya sare ya mabao 2-2 na Zimbabwe kwa kupiga mbili, kabla ya supastaa mwingine wa nguvu Afrika, Sadio Mane naye kutupia wavuni wakati Senegal ilipoichapa Tunisia 2-0.

Mwanzo huo mzuri kwa wanasoka hao wanaocheza klabu kubwa kabisa za Bara la Ulaya zinazidisha utamu kwamba, vita ya kusaka Kiatu cha Dhahabu kwenye Afcon 2017 itakuwa ya kukata na shoka.

Tayari Mane anayekipiga kwenye kikosi cha Liverpool ameshatupia moja, Aubameyang wa Borussia Dortmund ametupia moja na Mahrez wa Leicester City, naye ameweka kambani mara mbili.

Kutokana na hilo, Mahrez, ambaye ni Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika ndiye kinara wao kwa mabao, akiwa amepachika wavuni mara mbili.