Klopp amshangaa Mourinho kulalamikia ratiba

Saturday March 18 2017

 

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemshukukia Jose Mourinho kutokana na kulalamikia ratiba ya Manchester United kuwa mechi zake zimesongamana.

Wiki hii Mourinho alionyesha hisia zake akisema kwamba anatakiwa kukabiliana na Middlesbrough kesho huku akitakiwa tena kucheza mchezo wa robo fainali baada ya Ligi ya Europa.

Klopp alisema kwamba hata yeye msimu uliopita aliwahi kukutana na hali kama hiyo na akamshauri kocha huyo kwamba jambo la msingi ni kuwa tayari kukabiliana na ratiba ya mashindano hayo ya barani Ulaya.