Ghana yakana kugomea hoteli

Muktasari:

Ripoti zinafichua kwamba Ghana baada ya kuwasili katika ji wa Port-Gentil wakitokea Dubai, waliona wamekosewa heshima baada ya kuwekwa kwenye hoteli yenye hadhi ndogo Jumamosi iliyopita na kuomba wabadilishiwe.

CHAMA cha soka cha Ghana kimekanusha ripoti kwamba timu ya taifa ya nchi hiyo, Black Stars imegomea hoteli huko kwenye fainali za Afcon 2017 zinakazofanyika Gabon.

Ripoti zinafichua kwamba Ghana baada ya kuwasili katika ji wa Port-Gentil wakitokea Dubai, waliona wamekosewa heshima baada ya kuwekwa kwenye hoteli yenye hadhi ndogo Jumamosi iliyopita na kuomba wabadilishiwe.

“Ghana haijakataa hoteli yoyote waliyoandaliwa na Caf. Black Stars ipo na hizo ni habari za uongo,” ilibainisha taarifa ya FA ya Ghana.

“Ghana haijagomea uwanja wa mazoezi pia. Timu iliwasili usiku na kutokana na hali ya mazingira ya uwanja tofauti na ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari.”

Ghana itakipiga leo Jumanne kwa kumenyana na Uganda katika kundi lao kabla ya Mali kukipiga na Misri.

Ghana wanafukuzia kumaliza ukame wao wa miaka 35 ya kubeba taji hilo la Afrika ikiwa na mastaa wake kadhaa inaowategemea akiwamo Andre Ayew.