David Beckham akaribia kuwa Sir

Tuesday November 12 2013

LONDON, ENGLAND

KAMPUNI ya kuchezesha kamari ya Ladbrokes, imesimamisha kuchezesha kamari kuhusu uwezekano wa kiungo wa zamani wa Manchester United na England, David Beckham, kuteuliwa kuwa Sir mapema mwakani.

Staa huyo wa zamani wa Man United, Real Madrid, AC Milan, PSG na LA Galaxy, anaonekana kuongoza katika orodha ya watu wanaodhaniwa wanaweza kupewa cheo hicho katika siku ya mwaka mpya mwakani.

“Imekuwa suala la Beckham kuwa au kutokuwa katika nafasi hii, lakini baada ya kuona watu wengi wanaleta pesa zao katika kipindi cha saa 24 zilizopita tumeamua kusimamisha hilo kwa Sir David,” alisema Jessica Bridge wa Ladbrokes.

Mastaa wengine wanaopewa nafasi ya kuikwaa nafasi hiyo ni pamoja na AP McCoy, mwanariadha mwenye asili ya Somalia, Mo Farah, Mwanamuziki, Rod Stewart, mchekeshaji Billy Connolly na mpiga gitaa maarufu, Eric Clapton.