Arsenal watamu, hao namba mbili

Muktasari:

  • Bao la kichwa la kipindi cha pili lililofungwa na beki wa kati, Shkodran Mustafi, aliyefunga akiunganisha kona ya Mesut Ozil

LONDON, ENGLAND. LIGI Kuu England ina raha yake asikwambie mtu. Kwa mfano, cheki Arsenal walivyopanda kutoka nafasi ya nne hadi ya pili baada ya ushindi mmoja tu wakati jana Jumapili walipoichapa Burnley 2-1 kwenye Uwanja wa Emirates.

Bao la kichwa la kipindi cha pili lililofungwa na beki wa kati, Shkodran Mustafi, aliyefunga akiunganisha kona ya Mesut Ozil lilionekana kama ndilo lingekuwa pekee kwenye mechi hiyo, kabla ya kushuhudiwa penalti mbili ndani ya dakika za majeruhi, Burnley wakisawazisha kupitia kwa Andre Gray, ikionekana kama mechi itaisha kwa sare, Arsenal na wao wakapata penalti, Alexis Sanchez akatupia wavuni na kuifanya timu hiyo inayonolewa na Arsene Wenger kushinda na kufikisha pointi 47 zinazowafanya washike namba mbili kwenye msimamo pointi tano nyuma ya vinara Chelsea, ambao usiku wa jana walikuwa na mechi dhidi ya Hull City uwanjani Stamford Bridge.Mchezo mwingine wa ligi hiyo, Southampton iliendeleza mwaka mbaya kwa mabingwa watetezi, Leicester City baada ya kuwachapa 3-0.