Nusura Ronaldo acheze Birmingham

Monday December 29 2014Christian Ronaldo

Christian Ronaldo 

By LONDON, ENGLAND

MMILIKI mwenza wa Klabu ya West Ham United, David Sullivan, amesema kuwa walikaribia kumsajili nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ili aichezee Birmingham City.

Akizungumza katika kipindi kimoja cha televisheni, Sullivan, aliyekuwa mmoja wa mabosi wa Birmingham wakati huo, alisema klabu hiyo ilitoa ofa ya Pauni 6 milioni kumnasa Ronaldo mwaka 2003, staa huyo alipokuwa akiichezea klabu ya kwao Ureno, Sporting Lisbon. Hata hivyo, mchezaji huyo akaamua kujiunga na Manchester United.

“Kabla hajaenda Man United, tulimpa ofa ya Pauni 6 milioni, lakini akaachana na sisi na kujiunga na United,” Sullivan alisema.

“Kulikuwa na uwezekano wa dili letu kufanikiwa. Wakati ule alipoamua kwenda United kulikuwa na mashaka mengi dhidi yake, hakuwa nyota tofauti na ilivyo sasa.”