HATOKI MTU HAPA: Torres auzwa jumla AC Milan

Monday December 29 2014Fernando Torres

Fernando Torres 

By MILAN, ITALIA

AC Milan sasa inaonekana imenogewa na straika wa Chelsea aliye kwa mkopo klabuni hapo, Fernando Torres, kwani ina mpango wa kumsajili jumla wiki ijayo.

Torres aliwasili Milan mwezi Agosti kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili na amehusishwa mno na habari za kurejea klabu yake ya kwanza, Atletico Madrid. Lakini juzi Jumamosi Chelsea ilitangaza kuwa makubaliano yamefikiwa ili mchezaji huyo kusajili rasmi na Milan kuanzia Januari 5.

Hata hivyo mkataba huo hautainyima Atletico nafasi ya kumpata Torres mbeleni. Mabingwa hao wa Hispania wamesema kwamba hawana fedha za kumchukua jumla kwa sasa, lakini wanaweza kumchukua kwa mkopo kutoka Milan baada ya kuhamishwa kutoka Chelsea.