BADO MTAMU: Michael Carrick kuendelea kuula Man United

Mkali wa pasi kutokana na kiwango chake kizuri, Michael Carrick pia ameweza kurejea katika kikosi cha England mwaka huu.

Muktasari:

Carrick alikubaliana na kiwango hicho aliposaini mkataba wa kwanza mwaka jana na ameelezea kufurahishwa kwake kubakia klabuni hapo.

MANCHESTER United itaurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wa Michael Carrick unaompa Pauni 130,000 kwa wiki ili kumbakiza kiungo Old Trafford hadi baada ya majira ya joto.

Carrick alikubaliana na kiwango hicho aliposaini mkataba wa kwanza mwaka jana na ameelezea kufurahishwa kwake kubakia klabuni hapo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, amekuwa mmopa wa wachezaji muhimu kikosini humo tangu arejee kutoka benchi la majeruhi na mchango wake umesaidia kuifanya United kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Kocha, Louis van Gaal, anataka kubakia na Carrick na United inatarajiwa kuweka kila kitu wazi saa chache baada ya mwaka mpya kuanza.

Kutokana na kiwango chake kuzuri, Carrick pia ameweza kurejea katika kikosi cha England mwaka huu. Ana rekodi ya vikombe vitano vya Ligi Kuu England tangu alipohama Tottenham mwaka 2006 na alikuwa Mwanasoka Bora wa United mwaka jana.

United inaendelea kumkosa Marouane Fellaini katika msimu huu wa sikukuu baada ya kubainika kuwa Mbelgiji huyo aliumia mbavu katika mechi ya ushindi dhidi ya Liverpool wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo klabu hiyo ina habari njema za majeruhi wengine. Daley Blind na Marcos Rojo wanaendelea vizuri na wanaweza kucheza sawa na ilivyo kwa beki wa kushoto, Luke Shaw.